Licha ya kutokuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Yanga kwenye msimu uliomalizika hivi karibuni, Kpah Sherman aligeuka kivutio kwa mashabiki wengi waliojitokeza uwanja wa Karume jana kushuhudia mazoezi ya mabingwa hao.
Mashabiki wengi walimlaki na kumshangilia mshambuliaji huyo raia wa Liberia ambaye jana aliwasili mazoezini kwa mara ya akitokea nchini kwao alikokuwa kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa ligi.
“Nashukuru nimefika salama, nafurahi kuwa hapa tena. Yanga imekuwa ni nyumbani kwangu, nimefurahishwa mno na mapokezi niliyoyapata najiona mwenye deni kwa mashabiki wa Yanga na nimejiandaa kikamilifu kuipigania klabu yangu”, alisema Sherman.
0 comments:
Post a Comment