Na Ramadhani Ngoda,
Licha
ya baadhi ya wanazi wa Arsenal kufurahishwa na tetesi za kutua Emirates kwa
winga wa Liverpool Raheem Sterling, veterani wa klabu hiyo, Rey Parlour meibuka
na kukandia suala la kumuhitaji mchezaji huyo.
Kumekuwepo
na tetesi za Arsenal na Liverpool kubadilishana wachezaji Raheem Sterling na
Theo Walcott na kuibua mjadala mkubwa juu ya sakata hilo.
Licha
ya tetesi hizo, kiungo huyo wa zamani wa Arsenal haoni ujio wa Sterling kama una
manufaa na faida kwa timu hiyo ya Kaskazini mwa London.
Parlour
anaona Arsenal wanahitaji kufanya marekebisho katika nafasi mbalimbali kama
kiungo wa kati, beki na mshambuliaji wa kati lakini sio Raheem Sterling.
“Ningejikita
Zaidi katika kiungo wa kati, beki wa kati, mshambuliaji au golikipa kama
ningekuwa kocha,” alisema Palour.
Uwezekano
wa dili la kubadilishana wacheaji hao huenda pia likakwamishwa na kiwango
alichoonesha Walcott katika mchezo dhidi ya Westbrom aliopachika mabao matatu lakini
pia akifunga bao moja kati manne katika mchezo wa fainali ya kombe la FA dhidi
ya Aston Villa.
Arsenal
wanaonekana kuwa katika mawindo ya wachezaji mbalimbali katika kuboresha kikosi
chake wakiwemo Karim Benzema(Real Madrid), Arturo Vidal(Juventus), Edinson Cavani(PSG)
na Arsene Wenger analazimika kuingia mfukoni ili kukamilisha sajili hizo.
Kitendo
cha Madrid kubadili mfumo katika safu yake ya ushambuliaji kwa kumuweka Gareth
Bale kama mshambuliaji wa kati kunaweza kuchagiza upatikanaji wa mshambuliaji Karim
Benzema anayeonekana kuwa mbali na mipango ya kocha Rafa Benitez.
Hali
ya uchumi ya washika bunduki hao katika miaka ya hivi karibuni pia inaongeza
uwezekana wa kuona sura mpya nyingi katika klabu hiyo.
“Hali
ya uchumi kwa sasa ni nzuri Zaidi ukilinganisha na ya miaka mitano hadi sita
iliyopita. Kuwapata Mesut Ozil na Alexis Sanchez katika kipindi cha miaka
michache iliyopita kunaonesha jinsi gani Arsene Wenger hahofii kusajili
wachezaji wanaoonekana kuwa na msaada kwa timu,” aliongeza Parlour.
Arsenal
waliomaliza nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Chelsea na Manchester City
waliomaliza wa pili, wanahitaji kutengeneza kikosi cha ushindani Zaidi kwa
ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Uingereza na Ligi ya mabingwa barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment