Monday, June 8, 2015

EMMANUEL Okwi amewatikisa washambuliaji nyota hapa nchini, wakiwamo Amissi Tambwe na Simon Msuva walioibuka wafungaji bora misimu miwili iliyopita, baada ya Mganda huyo kuapa tuzo hiyo kutua Msimbazi msimu ujao.
Okwi kwa sasa yupo nchini kwao Uganda kwa mapumziko baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara mwezi uliopita, ikiwa ni baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu yake ya Simba na kushika nafasi ya tatu, japo ilianza vibaya ligi hiyo.
Pamoja na mapumziko, Okwi pia yupo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda, The Cranes, inayojiandaa na mechi za michuano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na ile ya wachezaji wa ndani (CHAN).
Akizungumza na BINGWA kutoka Uganda, Okwi alisema pamoja na kuwa mapumziko na majukumu ya The Cranes, akili yake ipo katika kuifanyia makubwa Simba msimu ujao.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video