Leo Jumamosi, Juni 13, 2015, kuanzia saa 3.00 asubuhi, katika Ukumbi wa U/taifa, Dar es salaam, viongozi wa Klabu za Ligi daraja la kwanza (FDL), 2015, tutakuwa na mkutano mkubwa wa kihistoria kujadili changamoto zilizopo katika ligi ya FDL na kuzitafutia ufumbuzi ili kuuboresha mpira wetu, uchezwe kwa ubora na viwango, uweze kukidhi kiu ya Tanzania.
Mgeni rasmi tumemwalika Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Juma Nkamia (mb).
Wageni wengine walioalikwa na wamethibitisha kuhudhuria ni;
M/kiti wa BMT
Rais wa TFF
M/kiti Bodi ya Ligi.
Rais wa TFF
M/kiti Bodi ya Ligi.
Wanahabari na Watanzani, Wadau, Wapenzi na Washabiki wa soka, karibuni tushiriki pamoja katika kuboresha soka letu ili tuachane na dhana ya "Kichwa cha mwendawazimu"
Imetolewa na Masau Bwire
Katibu na Msemaji Mkuu wa Klabu za FDL, 2015/16.
Katibu na Msemaji Mkuu wa Klabu za FDL, 2015/16.
0 comments:
Post a Comment