BINGWA wa dunia wa ngumi za uzito wa juu 'heavyweight', Deontay Wilder anaamini anaweza kurithi mikoba ya Floyd Mayweather Jr ya kuwa mwanamasumbwi anayetisha zaidi duniani.
Mmarekani huyo amefanikiwa kutetea ubingwa wa WBC katika ardhi ya Alabama, Marekani baada ya kumtandika bondia Eric Molina mwishoni mwa juma lililopita.
Licha ya kuwepo kwa mabondia bora wa dunia wakiwemo mabingwa wa ngumi za uzito wa juu wa IBF, WBA na WBO kama vile Wladimir Klitschko, Anthony Joshua , Wilder anaamini yeye ndiye bondia bora zaidi duniani.
Bondia huyo mwenye miaka 29 amesema: "Floyd Mayweather anaelekea kumaliza maisha yake ya ngumi. Inabidi nichukue nafasi yake. Naamini naweza kuwa bondia mpya mwenye mvuto zaidi duniani"
0 comments:
Post a Comment