Thursday, June 4, 2015



Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
MCHEZAJI tegemeo wa Taifa Stars, Mbwana Samata, amesema atarejea nchini na kuichezea moja ya klabu za Tanzania baada ya miaka 20 ijayo.

Samata ameyasema hayo jijini hapa leo akibainisha kuwa hana mpango wa kucheza katika klabu za Tanzania kwa sasa hadi pale atakapotimiza ndoto zake.

Amesema baada ya miaka hiyo 20, atakuwa ameshatengeneza maisha yake, hivyo utakuwa muda mwafaka kwake kurejee nyumbani.

"Baada ya miaka 20 ninaweza kurejea Tanzania na kucheza katika moja ya timu za hapa. Nitacheza hata bure kwa sababu nitakuwa nimeshatengeneza maisha yangu," amesema Samata.

Samata alizaliiwa Januari 7, 1992 jijini hapa, hivyo baada ya miaka 20 ijayo atakuwa na umri wa miaka 43, umri ambao ni wazi hatakuwa na uwezo mkubwa wa kusakata kambumbu.

Mkali huyo wa kufumania nyavu, kwa sasa anaitumikia TP Mazembe ya DRC. Timu nyingine alizowahi kuzitumikia ni African Lyon na Simba.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video