Joseph Tetteh Zutah pamoja na Donald Ngoma wanasaini mikataba yao asubuhi hii kwa ajili ya kuitumikia klabu ya Yanga baada ya jana kufuzu vipimo vyao vya afya.
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Dkt. Jonas Tiboroha mesema, wachezaji hao wanasaini mikataba yao asubu hii ili waendelee kupewa majukumu yao mengine wakiwa kama wachezaji halali wa Yanga.
“Vipimo vimekwenda vizuri kabisa kama tulivyokuwa tunatarajia, vijana wako fiti wamefaulu wote vizuri ‘with flying colors’ na vipimo vilichukua takribani siku nzima kuanzia saa 2:00 asubuhi mpaka saa 10:00 jioni”, amesema Tiboroha.
“Sasa tunasubiri kumaliza kilakitu asubuhi hii ili vijana waendelee na mambo mengine kama wachezaji kamili wa Yanga”, ameongeza.
“Huyu Mghana kidogo anacheza namba nyingi na ndio maana mwalimu alikuwa anamuhitaji sana kwasababu ni mchezaji anaeweza akacheza kama mlinzi wa kulia au kushoto lakini pia anaweza akacheza winga vizuri pamoja na ‘midfield’ kwa upande wa Ngoma yeye ni mshambuliaji”, amefafanua.
Wachezaji wanao mwaga wino Yanga asubuhi hii ni Donald Ngoma wa Zimbabwe na Joseph Tetteh Zutah kutoka Ghana.
0 comments:
Post a Comment