Saturday, June 6, 2015


Straika mkongwe anayerejea kuichezea Simba, Mussa Mgosi, amesema kwa namna yoyote ile, ni lazima avae jezi namba 11 klabuni hapo ambayo inavaliwa na Ramadhan Singano ‘Messi’.

Mazungumzo ya Mgosi na Simba kuhusu kujiunga na timu hiyo yapo katika hatua nzuri na muda wowote atasaini mkataba wa kuichezea timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar.
Mgosi aliliambia Championi Jumamosi kuwa, mara zote anapokuwa katika timu anayochezea hata kwenye ‘ndondo’, hupenda kuvaa jezi namba 11 akiamini ina mafanikio kwake.

“Siwezi kuzungumza mengi kuhusu Simba kwani tupo katika hatua nzuri na nina imani nitakuwa nao msimu ujao, kuhusu jezi mimi napenda kuvaa namba 11 na ndiyo nitakayoivaa Simba,” alisema Mgosi ambaye amemaliza mkataba na Mtibwa.


Hata hivyo, Mgosi anaweza akajichukulia kiulaini jezi hiyo namba 11 kwani Messi kwa sasa yupo katika malumbano na uongozi wa Simba kuhusu muda wa mkataba wake kwani mwenyewe anasema umeisha huku uongozi ukisema bado ana mwaka mmoja zaidi.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video