Na Ramadhani Ngoda,
Mshambuliaji wa Kimataifa wa Brazil na klabu ya FC
Barcelona, Neymar Jr amelazimika kuiaga michuano ya Copa America inayoendelea
baada ya kufungiwa michezo mine (4) na
kamati ya nidhamu ya chama cha soka cha Amerika Kusini kutokana na utovu wa
nidhamu aliyouonesha katika mchezo dhidi ya Colombia ulioshuhudia Brazil
ikilala bao 1-0 siku ya jumatano (tarehe 17/6/2014)
Mwamuzi Enrique Osses (kulia) akimuonesha kadi nyekundu nyota wa Brazil Neymar huku akitolewa nje na maafisa wa mchezo huo. |
Neymar alionekana akimbabua na mpira mchezaji wa Colombia
Pablo Armero baada ya mchezo kumalizika ndipo mwamuzi wa mcheoz alipomuonesha
kadi nyekundu licha ya kipyenga cha mwisho kuwa kilikwisha pulizwa kuashiria
kumalizika kwa mchezo huo.
Licha ya kosa hilo Neymar alishuhudiwa pia akimpiga kichwa
mchezaji mwingine wa Colombia Jeison Murillo katika mchezo huo huo.
Neymar (katikati) akimpiga kichwa mchezaji wa Colombia Jeison Murillo (mwenye jezi namba 22 na pamba puani) katika mchezo wa Copa America wa hatua ya makundi kati ya Colombia na Brazil. |
Mbali na kufungiwa michezo minne, Neymar anatakiwa kulipa
faini ya dola za kimarekani elfu kumi (10,000) kama sehemu ya adhabu
iliyotolewa lakini Brazil wamepewa nafasi ya kukata rufaa kama hawataridhishwa
na maamuzi hayo.
Brazil wanatarajiwa kucheza mchezo wao wa mwisho wa hatua ya
makundi dhidi ya Venezuela siku ya Jumapili na kama watafanikiwa kupita basi
hawatacheza michezo Zaidi ya mitatu katika hatua zinazofuata (robo fainali,
nusu fainali na fainali) jambo linaloondoa kabisa uwezekano wa staa huyo
kuonekana tena katika michuano hiyo kwa mwaka huu.
Brazil bado wana kibarua kutokana na kufungana point na Venezuela, Peru na Colombia kuelekea katika michezo ya mwisho ya hatua ya makundi.
0 comments:
Post a Comment