BAADA ya kucheza kwa mafanikio msimu wa 2014/2015 akitwaa makombe matatu, Mshambuliaji hatari wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi ametupia picha mtandao akiwa na mwanae Thiago pamoja na wazazi wake.
Mwishoni mwa juma lililopita, Messi alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Barcelona walioitandika Juventus mabao 3-1 katika mechi ya fainali ya Uefa Champions League na kufanikiwa kutwaa kombe la tatu ndani ya msimu mmoja ikiwa ni mara ya pili kihisitoria.
Barca msimu huu wametwaa La Liga, Copa del Rey na Uefa, wakati mahasimu wao wa jadi, Real Madrid wametoka 'ziro'.
0 comments:
Post a Comment