Omega Seme (kushoto)
Baada ya kunusurika kushuka daraja msimu uliopita, klabu ya Ndanda FC, inaendelea na mawindo ya usajili ili kupata kikosi cha maana kitachowasha cheche msimu ujao chini ya kocha mpya, Jumanne Chale.
Msemaji wa Ndanda, Idrissa Bandali amesema wamewaongeza mikataba wachezaji wao watano ambao wanaona bado wana umuhimu kikosini.
Amewataja wachezaji hao ambao wote wamesaini mwaka mmoja mmoja kuwa ni Wilibert Mweta, Kigi Makasi, Kasian Ponela, Hemedy Khoja na Masoud Ally.
Pia wamemsajili moja kwa moja kiungo Omega Seme aliyekuwa anacheza kwa mkopo kutokea klabu ya Yanga na amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment