Mshambuliaji mkongwe Gaudence Mwaikimba ametua JKT Ruvu iliyopania kujiimarisha ili ifanye vizuri msimu ujao.
Mwaikimba aliyekuwa akikipiga Azam FC, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea JKT Ruvu.
Mbele ya Makamu Mwenyekiti wa JKT, Meja Hassan Mabena Mwaikimba amemwaga wino, tayari kwa msimu ujao.
Tayari JKT imefanikiwa kumsainisha mshambuliaji Saad Kipanga kutoka Mbeya City.
JKT wamepania kukiboresha kikosi chao ili kufanya vizuri zaidi msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment