Luhende (kushoto)
Timu ya soka ya Mwadui ya mkoani Shinyanga iliyopanda daraja
hivi karibuni, imeionyesha Yanga kuwa nayo ipo vizuri kifedha na inaweza
kushindana nayo katika vita ya usajili ambayo inazidi kushika kasi hapa nchini.
Ijumaa iliyopita Mwadui FC ilifanikiwa kumsajili aliyekuwa
beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, David Luhende ambaye pia alikuwa akiwaniwa na
mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga, waliokuwa wakitaka kumrudisha kundini ili
waweze kuongezea nguvu kwenye safu yao ya ulinzi.
Inadaiwa kuwa Yanga ilikuwa imemtengea Luhende kitita cha
shilingi milioni 8 ili iweze kuipata saini yake lakini Mwadau FC iliingilia
kati na kuweza kuipiku klabu hiyo baada ya kumwekea mezani nyota huyo Sh
milioni 10.
“Tunamshukuru Mungu ndugu yetu kapata timu ambayo imeonyesha
kumjali na kuithamini kazi yake baada ya Mwadui kuamua kumpatia mkataba wa
mwaka mmoja kwa kitita cha Sh milioni 10 lakini pia atakuwa akilipwa mshahara
wa shilingi milioni moja kwa mwezi.
“Uamuzi huo wa Mwadui tumeupokea kwa mikono miwili na
imeonyesha kuwa, wapo vizuri kifedha kwani wameweza kuipiku Yanga ambayo pia
ilikuwa na nia ya kutaka kumrudisha kundini ila kiasi cha fedha walichokuwa
wamemtengea kilikuwa ni kidogo sana,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Hata hivyo, Luhende amesema kuwa anajiona ni mwenye bahati
na atahakikisha anaitumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote kwa sababu soka
ndiyo kazi yake inayomfanya aishi vizuri na familia yake.
0 comments:
Post a Comment