kerr (kushoto) akiwa na kocha mpya wa makipa wa timu hiyo, Abdul Iddi Salim (kulia) baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jioni ya leo tayari kuanza kazi Msimbazi.
Kocha mpya wa Simba, Dylan Kerr ametua leo mchana jijini Dar es salaam tayari kuanza kazi ya kuiandaa timu kwa ajili ya ligi kuu soka Tanzania bara.
Kocha mpya wa Simba akiongea na waandishi
Kerr, raia wa Uingereza ana uzoefu wa zaidi ya miaka 30 katika fani ya mpira wa miguu huku pia akiwa na umahiri wa kufundisha klabu mbalimbali duniani zikiwemo Hai Phong FC Vietnam, Hamilliton Academicals FC na Greennock Morton FC zote kutoka Scotland.
Kerr pia ana uzoefu wa kufundisha na kufanya kazi Afrika, ameshawahi kufanya kazi na kufundisha timu za South Africa NFD Nathi Lions FC na South Africa Thanda Royal Zulu FC kutoka Afrika Kusini
Kerr ana leseni ya daraja A na B ya ukocha aliyotunukiwa na Shirikisho la soka la Ulaya (UEFA) huku pia akiwa na uzoefu wa utawala katika fani ya michezo.
0 comments:
Post a Comment