Kiungo wa Simba, Jonas Mkude ameanza majaribio katika klabu ya Bidvest ya Afrika Kusini lakini ana kazi ya ziada kuonyesha kiwango cha juu zaidi kuliko Mrundi Papy Faty.
Faty ni Mrundi anayecheza soka katika klabu hiyo ya Afrika Kusini na ndiye amekuwa tegemeo katika uchezeshaji na ukabaji.
Hivyo lazima Mkude apambane kuonyesha atakuwa na kiwango cha Faty au zaidi.
Faty alijiunga na timu hiyo mwaka 2012 akitokea APR ya Rwanda na amekuwa tegemeo katika kiungo cha timu hiyo.
Hivyo ni lazima kwa Mkude kuwashawishi Wasauz hao kwamba ana uwezo wa juu hata kama ni baadaye baada ya kutengenezwa, lakini waone kitu ndani yake.
Tayari ameanza mazoezi kupambana kupata nafasi ya kuichezea klabu hiyo inayomilikiwa na Chuo Kikuu kongwe cha Wits.
0 comments:
Post a Comment