Tuesday, June 16, 2015

Inaikumbuka ile ishu ya Simon Msuva kufuzu majaribio ya kucheza soka la kulipwa katika klabu ya Bidvest Wits inayoshiriki ligi kuu ya Afrika kusini?

Mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu wakati ligi kuu soka Tanzania bara  ikielekea ukingoni, winga wa Yanga, Simon Msuva alialikwa kufanya majaribio Bidvest Wits ya Afrika kusini na akaripotiwa kufuzu, lakini kilichokwamisha kutua Bondeni ni mkataba wake wa mwaka mmoja na nusu ndani ya kikosi cha Wanajangwani.
Msuva amekiri kwamba mipango ya kuondoka bado haijakaa sawa kwasababu Bidvest Wits wanatakiwa kuonana na Yanga ili kuzungumzia uhamisho wake.
"Mipango inaendelea, wale jamaa (Bidvest) wanatakiwa kukutana na Yanga, wajue Yanga wanahitaji kiasi gani. Bado nina mkataba na Yanga, wanatakiwa kuzungumza na Yanga, wakimalizana naenda, sina uhakika kama nitabaki au nitakwenda, ila kwasasa mipango bado haijakaa sawa". Amesema Msuva.
Nyota huyo mwenye kasi uwanjani alishinda tuzo ya Mfungaji bora na mchezaji bora VPL 2014/2015 na kuhusu mafanikio hayo amesema: "Namshukuru Mungu kupata hizo tuzo, bila wachezaji wenzangu, viongozi kunipa sapoti nisingefanikiwa, ni jambo linalotia faraja sana".

Msuva alifunga magoli 17 na kushindwa kufikia rekodi ya Amisi Tambwe aliyefunga magoli 19 akiichezea Simba  msimu wa 2013/2014 wa ligi kuu soka Tanzania bara

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video