Klabu ya
Real Madrid ya nchini Hispania iko tayari kumuuza golikipa wao mkongwe Iker
Casillas huku wakikaribia kumnasa golikipa wa Manchester United, David de Gea.
Miamba hiyo
ya soka nchini Uhispania ina imani kuwa itampata golikipa David de Gea kutoka
Manchester United na kwamba wako tayari kumuuza golikipa na nahodha wa klabu
hiyo Iker Casillas kwa timu itakayokuwa tayari kutoa dau stahiki.
Iker
Casillas anatarajia kuondoka klabuni hapo mara baada ya kujulishwa kuwa atakua
golikipa namba 2 pindi usajili wa golikipa David de Gea utakapokamilika kutoka
Manchester United.
Tetesi
zinasema kuwa huenda kipa huyo akajiunga na klabu ya Tottenham Hotspurs ya
jijini London kutokana na uwezekano mkubwa wa kipa wa Spurs kutimkia Manchester
United inayojiandaa kuziba pengo la de Gea.
Inasemekana
kuwa kipa Iker Casillas anataka kujiunga na ligi kuu nchini Uingereza na hasa
jijini London, huku klabu ya Arsenal ikiwa pia inawania saini ya nahodha huyo
wa Hispania lakini kutokana na ukweli kwamba klabu ya Arsenal inamuwania pia
golikipa Peter Cech wa Chelsea, basi Casillas hawezi kuwa kipaumbele.
Real Madrid
haina haraka ya kumtaka David de Gea lakini wana imani kuwa golikipa huyo
atatua kwa mabingwa hao mara kumi wa Ulaya.
Wakati huo
huo mchezaji ghali zaidi duniani, Gareth Bale amehakikishiwa nafasi yake na
kocha mpya wa timu hiyo Rafa Benitez walipokutana wiki hii kabla ya mchezo wa
timu yake ya taifa Wales walipocheza na Ubeligiji. Inasemekana kuwa Kocha huyo
wa zamani wa Liverpool anatarajia kuijenga Real Madrid kupitia Gareth Bale.
Benitez
alitaka kumuonesha Gareth Bale ni jinsi gani yeye ni muhimu katika mipango yake
kabla ya kuanza kwa msimu mpya.
0 comments:
Post a Comment