John Tegete (kushoto) akiwa na mwanae Jerryson Tegete
SHIRIKISHO la soka Tanzania TFF bado linafikiria kukubali au
kukataa ombi la klabu na bodi ya ligi kuhusu kuongeza idadi ya wachezaji wa
kigeni kutoka watano hadi kufikia 10.
Klabu tatu kubwa nchini, Yanga, Azam, Simba zimetuma maombi
TFF zikitaka kuongezewa idadi ya wachezaji wa kigeni na kinachosubiriwa kwasasa
ni maamuzi ya kamati ya utendaji ya Shirikisho la soka nchini.
Wakati hayo yakiendelea, kocha wa Toto African ya Mwanza na
baba mzazi wa mshambuliaji wa Yanga aliyetimkia Mwadui fc, Jeryson Tegege, mzee
John Tegete amepingana na mawazo ya kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni
akidai inaua vipaji vya wazawa.
“Sikubaliani na suala la kuongeza wachezaji wa kigeni
kwasababu mpira wa Tanzania bado unasuasua na tutazidi kuua viwango vya
wachezaji Wazawa. Hata wachezaji watano waliopo sasa wanaua vipaji vya
wachezaji wetu. Timu zinawachezesha wachezaji wa kigeni kwasababu zinawalipa
fedha nyingi, lakini sio kwamba wana viwango zaidi ya wachezaji wazawa”.
Amesema Tegete na kufafanua: “England wanafikiria kupunguza idadi ya wachezaji
wa kigeni, sisi ambao hatupo hata kwenye ramani ya mpira tunataka kuongeza”.
“Timu tatu tu ndizo zinaweza kuleta wachezaji 10, vilabu
vingine haviwezi, huoni kama hii ni hujuma kwa nchi? Umewahi kuona wapi
wachezaji wa timu ya taifa wanachukuliwa kutoka Toto Africa, Mbeya City? wote
wanatoka timu tatu tu za Yanga, Simba, Azam na ndio maana timu ya taifa ni mbovu.
Hata marisevu wa timu hizo wanaitwa”………..
0 comments:
Post a Comment