Uongozi wa timu ya soka ya wakata miwa wa mkoani Morogoro Mtibwa Sugar umeendelea kulipiga ‘danadana’ suala la kocha atakaeinoa timu hiyo kuchukua mikoba ya Mecky Mexime ambaye amekalia ‘kuti kavu’ kunako timu hiyo.
Afisa habari wa klabu ya Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema, wapenzi na mashabiki wa timu hiyo wawe na subira wakati huu ambapo timu yao inafanya mipango ya kumpata kocha mpya kwa ajili ya kukinoa kikosi chao kwa majili ya simu ujao.
“Mimi nawataka wapenzi wa Mtibwa Sukari waendelee kuwa na subira, waendelee kuwa na utulivu wakai tukikamilisha masuala mazima ya mipango kabambe kwa ajili ya mimu wa 2015-2016 katika kinyang’anyiro cha ligi kuu Tanzania bara”, amesema.
“Tutazungumza na kuweka wazi suala la kocha mkuu muda si mrefu kutoka sasa na tuanajua wapenzi wa Mtibwa wanashauku ya kujua benchi la ufundi litaongozwa na nani. Hii ni kampuni na inamipango bora kabisa mimi nawataka waendelee kuwa na subira”, ameongeza.
“Mtibwa sio wageni wa ligi kuu Tanzania bara, tumekuwa kwenye hii ligi toka mwaka 1996 na tumecheza kwa mafanikio makubwa toka tuanze kucheza ligi mpaka kufikia sasa, ni moja ya timu yenye uzoefu, na mikakati kabambe. Tungeshateremka kama tungekuwa na mbinu ambazo si bora”, alitamba.
Mtibwa ina mpango wa kumsajili kocha wa kigeni ili aiongoze timu hiyo kwenye msimu ujao kutokana na kocha wao Mecky Mexime kuonekana kushindwa kutimiza malengo ya wakata miwa hao wa Manungu, Turiani.
0 comments:
Post a Comment