Na Ramadhani Nngoda
Ni kama kata mti panda mti kwa Chelsea ya Jose Mourinho.
Baada ya kubainika kuwa mlinda lango raia wa Jamhuri ya Czec, Petr Cech yu
mbioni kuondoka Stanford Bridge, Jose Mourinho anatazamia kuingia Stoke City
kumnyakuwa mlinda lango wa klabu hiyo Asmir Begovic na kumpeleka darajani.
Chelsea wamelazimika kuingia kwenye mazungumzo na Stoke kwa
ajili ya kupata saini ya Begovic na kuhakikisha anakuwa kipa namba mbili wa 'blues' nyuma ya Mbelgiji Thibaut Courtois.
Cech mapema aliiambia Chelsea kuwa anataka kwenda Arsenal na
kuna uwezekano mkubwa wa golikipa huyo kuichezea ‘The Gunners’ msimu ujao wa
ligi unaotarajiwa kuanza mwezi wa nane mwaka huu.
Inafahamika kuwa Mourinho anataka kipa wa kiwango cha juu
ili kutoa changamoto kwa Courtois kabla ya mabingwa hao watetezi wa Uingereza
kuidhinisha safari ya Cech kwenda Arsenal.
Begovic ambaye pia anawaniwa na vilabu mbalimbali barani
Ulaya ikiwemo Manchester United inayomuhitaji kama mbadala wa David De Gea
anayetazamiwa kuelekea Real Mdrid muda wowote, amemvutia Jose Mourinho licha ya
Mreno huyo kujua ugumu wa kupata saini yake kutokana na ukweli kuwa Begovic
asingependa kuwa mkalia benchi bali kupata nafasi ya kikosi cha kwanza kama
ilivyo Britania, lakini anaamini pesa inaweza kumshawishi mlinda lango huyo
kumwaga wino ‘The Blues’
Chelsea wako tayari kumwachia Cech lakini kwa sharti la
kupata mchezaji mmoja toka Arsenal.
0 comments:
Post a Comment