Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho bado anaendelea kulipiga danadana ombi la Arsenal wanaotaka kumsajili golikipa Petr Cech kwa dau la paundi milioni 11.
Washika Bunduki wa London wanahitaji dili hilo likamilike wiki hii, lakini wanakumbana na upinzani mkali kutoka kwa Mourinho.
Cech anataka kutua Emirates na inafahamika kwamba mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich hana mpango wa kumbakisha kipa huyo mwenye miaka 33.
Hata hivyo, Mourinho hataki kuwaimarisha wapinzani wake Arsenal kwa kumruhusu Cech kutua London.
Bosi huyo wa Chelsea ameomba Arsenal impatie Alex Oxlade-Chamberlain au Theo Walcott ili awape Cech - lakini Arsene Wenger amekataa mapendekezo hayo.
Mourinho anapenda kuona Cech anajiunga na Paris Saint-Germain, ambao pia wanavutiwa na huduma yake.
0 comments:
Post a Comment