Chidiebele
UONGOZI wa Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ unahaha kuinasa saini ya mshambuliaji hatari
wa Stand United ‘Chama la Wana’, Mnigeria, Abasalim Chidiebele ambaye amemaliza
mkataba na klabu yake yenye makazi yake mkoani, Shinyanga.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Coastal Union, Salim
Bawaziri amesema hawataki kukurupuka kwenye suala la usajili na wanasubiri safu
mpya ya uongozi itayoingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu utakaofanyika
Julai 5 mwaka huu.
“Mipango ya usajili inaendelea vizuri, unajua usajili una
mambo mengi sana, kuna kukaa na wachezaji na kuelewana nao juu ya mikataba yao.
Sisi tumetulia na hatutaki kukurupuka, nadhani viongozi watakapopatikana tutaanza
rasmi”. Amesema Bawaziri na kuongeza: “ Chidiebele (Abasilim) tunafanya naye
mazungumzo, tupo katika hali nzuri, tukimalizana naye tutamtangaza”.
Mbali na Coastal, timu za
Kagera Sugar na Mbeya City fc zipo kwenye windo la kumnasa Chidiebele
aliyefunga magoli 11 msimu uliopita wa
ligi kuu uliomalizika Mei 9 mwaka huu kwa Yanga kutawazwa mabingwa wapya
wa ligi kuu Tanzania bara.
Chidiebele mwenyewe amethibitisha kuwa kwenye mazungumza na
klabu tatu kwa maana ya Kagera, Mbeya City na Coastal, lakini bado hajafikia
makubaliano yoyote na amesisitiza kuihama Stand United akidai ina ubabaiuhaji mwingi.
0 comments:
Post a Comment