Sunday, June 7, 2015

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, 'The Cranes, 'Milutin 'Micho' Sredojevic amemtema mshambuliaji hatari wa Simba, Emmanuel Anord Okwi kwenye kikosi chake kitakachokabiliana na Gambia katika mechi ya kimataifa ya kirafiki pamoja na ya Botswana kuwania kufuzu AFCON 2017.
Pia mshambuliaji aliyevunjiwa mkataba na  Simba, Daniel Sserunkuma ameachwa kwenye kikosi hicho, wakati winga wa Azam fc, Brian Majwega  amejumuishwa.
Mshambuliaji wa zamani wa Azam fc, Brian Umony ameitwa kwenye kikosi hicho.
Uganda  'The Cranes' itachuana na Gambia juni 9 mwaka huu katika mechi ya kimataifa ya  kirafiki na jun 13 itacheza dhidi ya Botswana kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017.
Kuelekea katika mechi hizo, leo Micho ametangaza kikosi cha wachezaji 26
WACHEZAJI WANAOKOSEKANA;
Wanandinga wengi waliokuwa nguzo ya timu ya Uganda siku za nyuma wameachwa.
Tonny Mawejje, nahodha Andrew Mwesigwa, Moses Oloya, Geofrey Baba Kizito, Daniel Sserunkuma, Emma Okwi wote wameachwa kwasababu mbalimbali.
Kipa wa timu ya vijana ya Vipers SC, James Alitho ameitwa kwenye timu kubwa ya Taifa.
Brian Ochwo, Denis Okot, Shafiki Bakaki na John Semazzi ni vijana wengine waliojumuishwa kwenye kikosi hicho.
Pia kiungo wa ulinzi wa Kira , Derrick Tekkwo, ameitwa na Micho.
WACHEZAJI WANAOCHEZA SOKA LA KULIPWA
Wanasoka watatu wanaokipiga soka la kulipwa nchini Ethiopia, golikipa Robert Odongkara, Isaac Isinde na Brian Umony wamejumuishwa kwenye kikosi hicho.
Wachezaji wengine wanaocheza soka la kulipwa walioitwa ni mlinda mlango Denis Onyango (Mamelodi Sundowns), Geofrey Massa (Bloemfontein Celtics), Alex Kakuba (Estoril), Wiliam Luwagga Kizito (Sporting Colviha), Boban Zirintusa (Polokwane) Godfrey Walusimbi, Aucho Khaldi (Gor Mahia) na walinzi wawili wanaocheza Lebanon , Richard Kasagga na Denis Iguma.
Uganda inatarajia kucheza dhidi ya Gambia jumanne ijayo katika mechi ya kirafiki kabla ya kuchuana na Botswana jumamosi ya juni 13 kwenye mechi ya kundi D kuwania kufuzu AFCON 2017.
Mechi zote mbili zitachezwa uwanja wa Nelson Mandela, Namboole na kwasasa timu imeingia kambini katika hoteli ya Hoteli ya Sky.
KIKOSI KIZIMA HIKI HAPA
WALINDA MLANGO:
 Denis Onyango, Robert Odongkara, James Alitho 
WALINZI:
Isaac Isinde, Denis Iguma, Alex Kakuba, Denis Okot, Brian Ochwo, Richard Kasagga, Shafiq Bakaki, Hassan Wasswa
VIUNGO:
Derrick  Tekkwo, Khalid Aucho, Boban Zirintusa, Yasser Mugerwa, Kezironi Kizito, Farouk Miya, Saidi Kyeyune, William Luwagga Kizito, Godfrey Walusimbi na Brian Majwega 
WASHAMBULIAJI:
Geoffrey Massa, Robert Ssentongo, Brian Umony, Yunus Sentamu, John Semazzi 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video