Mshambuliaji mkongwe Mussa Hassan Mgosi, jana alianza rasmi
mazoezi na klabu yake mpya ya Simba kwa mkwara mzito ambapo amewaahidi
mashabiki wa timu hiyo kusubiri mambo mazuri kwa kuwaambia kuwa amerejea
Msimbazi kwa kazi na siyo maneno.
Mgosi aliyerejea SImba akitokea Mtibwa
Sugar alikuwa injini na kuwaongoza wachezaji chipukizi kwenye kila programu
katika mazoezi hayo yanayoendelea kwenye Gym ya Chang’ombe tangu Jumanne wiki
hii yakisimamiwa na kocha msaidizi, Selemani Matola.
Kuanza mazoezi katika siku ya kwanza tu imeonyesha kuwa
kweli Mgosi ni mmoja ya wachezaji wakomavu na wanaoyajua majukumu yao.
Kwani idadi ya walioanza mazoezi ni wachache sana ikionyesha
wengi wataingia mazoezini baada ya siku mbili tatu au nne.
Lakini mkongwe huyo amekuwa kati ya wale walioanza mazoezi
mapema jambo ambalo wengine wanapaswa kujifunza.
Source: Salehjembe
0 comments:
Post a Comment