Mchezaji Jonas Mkude wa Simba SC tayari yupo Afrika Kusini kwa majaribio katika klabu ya Bidvest Wits na taarifa zinasema amepokelewa vizuri na kuthaminiwa ipasavyo.
Mkude amefikia kwenye nyumba nzuri na kupiga picha pembeni ya magari ya maana.
Mkude ameendelea kuwaomba Watanzania wazidi kumwombea ili aweze kufuzu majaribio.
Mkude aliondoka akiwa na Baraka zote za Klabu ya Simba, Rais wa Simba Evans Aveva alisema “Simba inamtakia kila la kheri Mkude kwenye majaribio yake kwenye Klabu ya Bidvest Wits huko Afrika Kusini na hili liwe fundisho kwa vijana wengine kuendeleza vipaji ili waweze kucheza mpira kwenye ligi za Nchi nyingine kubwa hivyo kukuza upeo na vipaji Zaidi katika soka”. Alisema taarifa ya Simba.
Mkude alizaliwa Desemba 3, 1992 Kinondoni B na kuanza soka lake akiwa mlinda mlango hadi kuwa kiungo wa kutegemewa. Aidha alianza elimu ya msingi mwaka 1998 katika shule ya Hananasif na kumaliza mwaka 2005
0 comments:
Post a Comment