Friday, June 5, 2015

KATIBU  mkuu wa Mbeya City Fc,  Emmanuel Kimbe amewataka  mashabiki wa timu hiyo popote walipo duniani kutokuwa na wasiwasi wowote kuhusu majaaliwa ya kikosi chao msimu ujao wa ligi kuu Tanzania Bara, kufuatia kuondoka kwa nyota kadhaa waliokuwa sehemu ya mafanikio  kwa misimu miwili  iliyopita.
Akizungumza mapema leo na Tovuti rasmi ya klabu hiyo kwenye ofisi za timu zilizopo Mkapa Hall,  jijini Mbeya, Kimbe alisema kuwa  ni wazi kuondoka kwa nyota hao kumewashtua wengi , lakini kwenye soka mchezaji kuhama timu moja kwenda nyingine ni jambo la kawaida.
“Tulio wengi tumeshtuka lakini  kwenye soka hili ni jambo la kawaida, zipo timu zimewahi kuondokewa na wachezaji wengi na baadaye zikafanya vizuri, kikubwa ni maandalizi ya kikosi kipya ambacho kinakuwa kimeundwa baada ya walikuwepo kuondoka ” alisema.
Akiendelea zaidi Katibu Mkuu Kimbe alidokeza kuwa City inayo timu nzuri ya vijana ambayo imekuwa sehemu ya mafanikio kwasababu wachezaji wote wanaaopandishwa kutoka kwenye kikosi hicho cha U20 wamekuwa wakifanya vizuri  kwenye timu kubwa.
“Tuna timu nzuri ya U20, vijana wengi tumekuwa tukiwapandisha kutoka huko na wamekuwa sehemu ya mafanikio huku juu, mfano mzuri ni Rafael Daud, alipandishwa wakati wa dirisha dogo,  ameonyesha uwezo mkubwa , tunatarajia makubwa zaidi msimu mpya  kutoka kwake pamoja na wengine tutakaowapandisha safari hii”.
“Hivyo basi hakuna haja ya kuwa na hofu  kwa mashabiki wa timu yetu, naomba muamini timu itakuwa vizuri msimu ujao kupitia vijana wetu tunaowapandisha na pia wazoefu wachache tutakaowasajili kuja kusaidiana na waliopo. hii ndiyo soka kwa sababu sisi tunaweza kusajili mchezaji kutoka timu nyingine, ndivyo timu nyingine zinaweza kusajili kutoka kwetu, hili lisiwatie hofu, City itabaki kuwa City na hilo halitabadilika, alisema.
Kuhusu suala la kuisha kwa mikataba ya wachezaji  na wengine kuondoka, Kimbe alisema kuwa ni kweli mikataba ya wachezaji wao wengi ilikuwa inakwisha baada ya msimu na  kulikuwa na mazungumzo kabla na wachache kati yao walikubali kuongeza mikataba mipya na wengine walikataa.
“Hakukuwa na namna katika hili, tulizungumza nao mapema lakini waligoma, nadhani ni kwa sababu walitaka kuwa huru ili wafanye makubalino mapya kule wanakokwenda, tulijitahidi lakini waligoma kwa sababu tayari kulikuwa na shinikizo nyuma yao, kama klabu hatukuwa na njia nyingine ya kuwafanya wabakie, tunawatakia heri huko walikokwenda  kwa sababu soka ndivyo ilivyo”. alimaliza Kimbe.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video