Kikosi na Mbeya City Fc U20 kinatarajia kufanya ziara rasmi ya michezo kadhaa ya kirafiki mjini Sumbawanga kufuatia mwaliko wa kampuni moja ya michezo mjini humo.
Afisa habari wa Mbeya City Fc, Dismas Ten, mapema leo amesema kuwa City U20 itakuwa mjini Sumbawaga kwa michezo saba ya kirafiki na timu mbalimbali kutoka ukanda huo.
“Mwishoni mwa wiki hii vijana wetu watakuwa kwenye ‘Tour’ huko Sumbawanga tumepata mwaliko maalumu kutoka kampuni ya michezo inayongozwa na Mkurugenzi Ernest Mabona, tumekubali mwaliko huu kwa sababu hii sehemu nyingine nzuri ya kuwapima na kuwaimarisha nyota walio kwenye kikosi hiki alisema Ten,
Akiendelea zaidi Ten aliweka wazi kuwa ziara hii ya vijana hawa itakuwa ni kipimo kingine kizuri kwa nyota ambao wanatarajiwa kupandishwa kwenda timu kuwa na imekujwa wakadi mzuri ikiwa ni siku chache tu zimepita tangu kutolewa kwa mikwaju ya penalti kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Muungano wilayani Mufindi.
“Kucheza michezo saba ya kirafiki ni kipimo kizuri, tuna vijana wengi wazuri kwenye kikosi hiki ambao mwalimu anatarajia kuwapandisha kikosi cha kwanza msimu ujao, hii ni sehemu nyingine ya kupima uwezo wao hasa baada ya kutoka kwenye mashindano ya Muungano Mufindi” alisema.
0 comments:
Post a Comment