Na Ramadhani Ngoda.
Mlinda
lango wa Tottenham Hotspur na timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Lloris ameweka
wazi matamanio yake ya kutaka kucheza ligi ya mabingwa barani Ulya na kuzipa
nguvu tetesi za yeye kurithi mikoba ya David De gea anayetarajiwa kutimkia Real
Mdrid katika kipindi hiki cha usajili.
Lloris
(24) ni mmoja kati ya makipa waliounda orodha ya walinda lango wanaohitajika na
Man United kuchukua nafasi ya De gea anayeonekana kuwa karibu na mlango wa
kutokea Old Trafford na kurejea katika jiji la Madrid.
“Nadhani
kila mchezaji anapenda kucheza ligi ya mabingwa kwa sababu ndio kiwango cha juu
kabisa, tunatafuta hilo siku zote. Na
naamini nitacheza ligi ya mabingwa tena,” alinena Lloris.
Inafahamika
kuwa Lloris ni moja kati ya makipa bora kwa sasa na hii inarandana na ukweli
kuwa Mdachi Luis Van Gaal anakuna kichwa kusaka kipa anayeweza kuziba vema
pengo la De Gea licha ya kumsajili Victor Valdes kwa mkataba wa miezi 18 kutoka
FC Barcelona.
Mfaransa
huyo aliyesajiliwa na Spurs kutoka Lyon mwaka 2012 kwa ada ya pauni milioni 8,
licha ya shauku ya kucheza ligi ya mabingwa, hatalazimisha kuondoka White Hart
Lane kwa sasa kutokana na kuiheshimu klabu yake.
“Nina
mkataba mpaka 2019, na ninaheshimu uongozi, klabu pamoja na wachezaji wenzangu
hivyo nsingependa kuongelea hilo,” aliongeza Lloris.
Alipoulizwa
juu ya uwezekano way eye kumrithi David De gea Man Utd, Lloris alikataa kuweka
wazi msimamo wake kutokana na De gea kuwa bado ni mchezaji wa United kwa sasa.
“De
gea bado ni mlinda lango wa Manchester United kwa sasa, hivyo sioni haja ya
kulizungumzia suala hilo,” alisisitiza Mfaransa huyo.
Hugo
Lloris aliyewahi kuzichezea klabu za Nice na Olympic Lyon za Ufaransa kabla
kuhamia Uingereza, ameshaichezea Tottenham michezo 100 pamoja na michezo 65
aliyoitumikia timu ya taifa ya Ufaransa katika michuano tofauti tofauti.
0 comments:
Post a Comment