Kocha wa Juventus, Massimiliano Allegri hana namna ya kumzuia kiungo wake, Paul Pogba kama ataamua kuondoka kwa miamba hiyo ya Turin majira ya kiangazi mwaka huu.
Pogba ametoa mchango mkubwa katika makombe mawili ya nyumbani ya Juventus na kufika fainali ya Uefa Champions League msimu uliopita.
Klabu mbalimbali zikiwemo Manchester City, Barcelona na Paris Saint-Germain zinavutiwa na nyota huyo mwenye miaka 22.
"Uhamisho wa Pogba? kiuweli yatakuwa maamuzi yake kuondoka klabuni na si kwa sababu ya benchi la ufundi kuhitaji", Allegri amewaambia Gazzetta dello Sport.
"Lakini kama Paul atabaki Turini, anatakiwa awe ameamua kwa akili sahihi ili asije kujuta"
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa alijiunga na Juventus akiwa huru mwaka 2012 akitokea Manchester United na sasa anaripotiwa kuwa na thamani ya paundi milioni 80.
Pogba ni mchezaji hatari tangu atue Juventus na mkataba wake utamalizika Juni 2019.
0 comments:
Post a Comment