Siyo mara ya kwanza kutokea lakini hii ya safari hii inaweza
kuwa ni jibu. Unakumbuka mapema mwaka huu mashabiki wa Simba walilisukuma gari
la Emmanuel Okwi mara baada ya timu hiyo kupata ushindi dhidi ya JKT Ruvu
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam? Sasa straika wa Yanga amejibu.
Tukio hilo lilitokea kwenye Uwanja wa Karume mara baada ya mechi hiyo ya
kirafiki ambapo kundi kubwa la mashabiki wa Yanga liliisukuma gari kutoka ndani
ya uwanja mpaka nje huku likimshangilia kwa kuimba “Tambwe, Tambweee,
Tambweeeee!”
Jibu hilo limetoka kwa Mrundi, Amissi
Tambwe ambaye mashabiki waliamua kusukuma gari lake aina ya Toyota Brevis
kutokana na kufurahishwa na uwezo wake katika mechi dhidi ya Friends Rangers.
Mashabiki wengine walikuwa wakisafisha vioo vya gari hilo huku Tambwe
akiwapungia mkono.
Source: Salehjembe
0 comments:
Post a Comment