Kocha Mkuu wa Togo, Tom Saintfiet amecharuka kuhusiana na nyota wake, Emmanuel Adebayor kuchelewa kujiunga na wenzake.
Saintfiet aliyewahi kuinoa Yanga na kuipa ubingwa wa Kombe la Kagame amesema Adebayor ameonyesha utovu wa nidhamu.
Kocha huyo raia wa Ubelgiji amesema, Adebayor ameonekana siku mbili tofauti lakini hakwenda kambini kuungana na wenzake wanaojiandaa kuipigania Togo kufuzu Kombe la Mataifa Afrika.
“Kweli ni mchezaji muhimu, lakini si sahihi alichofanya na siwezi kufanya kazi na mtu asiyejali nidhamu.
“Tunapokuwa katiaka kikosi, basi kila mchezaji anakuwa sawa na mwingine, hakuna anayewazidi wengine hata kama atakuwa muhimu zaidi ya wengine,” alisema kocha huyo mkali katika suala la nidhamu tokea akiwa Yanga.
Togo inashuka dimbani nyumbani dimbani jijini Lome, Jumapili dhidi ya Liberia kufuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika.
0 comments:
Post a Comment
Links to this post
Create a Link