Sunday, June 14, 2015


Wakati maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara yakiendelea, timu ya Maiimaji FC ya Songea ‘Wanalizombe’  ambayo imepanda kucheza ligi kuu msimu ujao, katibu mkuu wake Zacharia Ngalemanayo ameamua kung’atuka kuipisha nafasi hiyo.
Kiungo huyo ameeleza kwamba amefikia uamuzi huo baada ya kuzidiwa na  majukumu ya kifamilia pamoja na majukumu mengine binafsi.
Ngalemanayo aliwasilisha barua kwa mwenyekiti wa klabu ya Majimaji akieleza sababu zilizopelekea aamue kujiuzulu, lakini moja ya sababu ambazo zimeonekana kuwa ni kubwa ni ile ya kukabiliwa na majukumu ya familia pamoja na majukumu binafsi.
 Barua hiyo ambayo iliwasilishwa kwenye kikao cha bodi ya timu hiyo na mwenyekiti wa timu Humphrey  Milanzi, baada ya wajumbe kutafakari kwa kina juu ya uamuzi huo waliridhia uamuzi wake na kutoa jukumu jingine tena kwa mwenyekiti kuona ni namna gani ya kufanya uteuzi wa katibu mpya.
Kulingana na majukumu ambayo klabu ya Majimaji inayo kwa sasa ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji na kufuatilia taarifa mbalimbali kutoka shirikisho la soka nchini, mwenyekiti aliwasilisha jina jingine la mtu ambaye amekiri kuziba pengo hilo ambaye ni Charles Mchanakutwa.
Hivyo kinachosubiriwa hivisasa ndani ya klabu ya Majimaji ni makabidhiano ambayo yatafanyika muda wowote kuanzia sasa kwasababu barua hiyo ya kujiuzulu kwa katibu huyo imewasilishwa na jina jipya tayari limeshapelekwa kwenye bodi ya klabu na kuridhia.
Majimaji imerejea kunako ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2015-2016 baada ya kuporomoka daraja na kusota kwenye ligi daraja la kwanza kwa misimu kadhaa. Ligi kuu msimu ujao itakuwa na timu 16 badala ya timu 14 zilizoshiriki ligi iliyomalizika hivi karibuni.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video