Nahodha wa Manchester United Wayne Rooney anaamini klabu yake itawania ubingwa wa EPL msimu ujao hasa kutokana na usajili ambao tayari umeshafanywa na unaoendelea kufanywa na kikosi chake.
Kikosi hicho chini ya Van Gaal, kilimaliza ligi kikiwa pointi 17 nyuma ya mabingwa wa ligi msimu uliopita klabu ya Chelesea lakini waliweza kumaliza ndani ya timu nne za juu na kukata tiketi ya kushiki michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) msimu ujao.
United tayari imeshamsajili winga wa Uholanzi Memphis Depay kwa ada ya uhamisho wa pauni milioni 25 kutoka klabu ya PSV na inamuwania mlinzi Sergio Ramos wa Real Madrid.

“Ukitazama kwenye mechi 10 za kwanza kati ya 11 tulikuwa na pointi 13 tu, na ukitazama tulipomaliza nafikiri inaonesha tungekuwa juu zaidi ya hapo kama tungeanza vizuri”, amesema.
“Tulitawala na kucheza vizuri kwenye mechi nyingi msimu huu, lakini hatukutumia nafasi hiyo kupata ushindi kwenye hizo mechi, ingekuwa ni stori nyingine kama tungekuwa tunashinda”.

“Itakuwa ni jambo jema kushinda vikombe vingi, klabu kama Manchester United inatakiwa kutwaa mataji na ninaamini tunaweza kufanya hivyo msimu ujao”
Rooney amesema, msimu uliopita ulikuwa ni wa kukatisha tama kwa mara nyingine tena kwa United kushindwa kunyanyua taji lolote na kuishia kumaliza ligi wakiwa mikono mitupu lakini akaongeza kuwa, kama wangeshindwa kumaliza ndani ya klabu nne za juu ‘top four’ ingekuwa ni ‘janga’.
Ameendelea kusema, “lengo letu kuu ilikuwa ni kumaliza ndani ya klabu nne za juu, na tulifaniwa katika hilo. Kwa maana hiyo sio mbaya sana”.
“Tunatakiwa kuelewa kwamba, mwanzoni mwa msimu tulikuwa na makocha wapya na wachezaji wengi wapya, kwa hiyo ilikuwa siyo rahisi kwa upande wetu kutwaa taji la ligi”.
0 comments:
Post a Comment