Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema ndiyo wanatengeneza kikosi na watu wanapaswa kuvuta subira.
Pluijm amewatumia karibu wachezaji wake wageni wote kwa ajili ya kuwaangalia katika mechi ya kirafiki dhidi ya SC Villa ya Uganda leo.
“Utaona mechi imeisha kwa sare ya bila kufungana licha ya kwamba hakukuwa na mabao, tumepata nafasi ya mkwaju wa penalty, lakini tumepoteza.
“Bado tunatengeneza timu na unaona namna vijana walivyoonyesha mchezo mzuri.
“Bado tuna mechi za kirafiki, muda wa mazoezi ambao pia utatupa nafasi ya kujua tuko vipi.
“Sasa ni mapema sana kujipima kwa kiasi cha kusema tuko vipi. Naweza kusema ulikuwa mwanzo mzuri,” alisema Pluijm.
Licha ya kujaza wachezaji wengi hasa mbele huku Deus Kaseke, Malimi Busungu na Geofrey Mwashyuya bado waliweza kuonyesha kiwango kizuri.
0 comments:
Post a Comment