Manchester
United inatarajia kupeleka ofa kwa ajili ya kumnasa mlinzi wa klabu ya Everton,
John Stones mwenye miaka 21 katika majira haya ya joto.
John Stones
ambaye hivi karibuni ataiwakilisha timu yake ya taifa ya uingereza chini ya
miaka 21 katika fainali za U21 za mataifa ya Ulaya amekuwa akitajwa kama mmoja
wa mabeki wenye uwezo mkubwa chipukizi.
Stones
ambaye ametajwa mara kadhaa na kocha Jose Mourinho wa Chelsea kuwa anaweza kuwa
mbadala wa John Terry kwa muda mrefu alisaini mkataba wa muda mrefu na klabu
yake ya Everton hadi mwaka 2019 wenye thamani ya pauni 30,000 kwa wiki.
Stones
amejiweka kuwa moja ya wachezaji muhimu wa klabu hiyo ya Merseyside huku
akicheza michezo 29 katika mashindano yote pamoja na awali kukumbwa na majeraha
yaliyo muweka nje ya uwanja kwa muda mrefu.
Kocha wa
Manchester United, Loius Van Gaal amemgeukia mlinzi huyo mwenye uwezo wa
kucheza mlinzi wa kati na kulia, mara baada ya kuwa na matatizo ya ulinzi hasa
wa kati tatizo lililojitokeza tangu kuondoka kwa walinzi Rio Ferdinand na
Nemanja Vidic misimu miwili iliyopita.
Aidha mlinzi
wa kati wa sasa wa Manchester United, Chris Smalling amesema anaamini yeye na
mlinzi mwenzake Phil Jones wanaweza kuwa mapacha wa kudumu katika eneo hilo la
moyo wa ulinzi la Manchester United. Lakini majeraha ya mara kwa mara ya Phil
Jones na kutokuwa na uwezo sawia kwa Chris Smalling kunatia shaka safu ya
ulinzi ya timu hiyo ambayo imefuzu kucheza michezo ya mabingwa wa Ulaya msimu
ujao baada ya kuikosa msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment