Na Ramadhani ngoda
Mashetani wekundu wa Old Trafford, Manchester United
wameitupilia mbali ofa ya Real Madrid ya pauni milioni 13 walioitoa kwa ajili
ya mlinda mlango wa klabu hiyo David De Gea na kuendeleza msimamo wao wa
kutomuuza mchezaji huyo kwa pesa iliyo chini ya pauni milioni 25.
Mabingwa hao wa Ulaya mara 10 wanaamini wanaweza kumsaini De
Gea na raisi wa klabu hiyo Fiorentino Perez yuko tayari kumaliza usajili huo
wiki hii lakini Manchester United wameionya Madrid kuwa wasitarajie kumnasa
Mhispania huyo wakiwa wamvaa ‘shati la ubakhili.’
Huku sakata la usajili wa De Gea likiendelea, mlinda mlango
wa zamani wa mashetani wekundu, Edwin Van De Sar amekuja juu na kusema kuwa Man
Utd wanaweza kuishi maisha ya bila De Gea na haoni sababu ya Utd kuendelea
kuumiza kichwa kumbakisha.
“Hakuna pengo lisilozibika, na hivyo ndivyo ilivyo siku
zote. Alikuja hapa akiwa kijana mdogo, amekulia hapa na kuwa kipa wa kiwango
cha juu sasa. Nina uhakika kama ataondoka Utd watapata mbadala sahihi,” alisema
Veterani huyo aliwahi kutwaa ligi ya mabingwa na matajiri hao wa Manchester.
Jeuri ya Real Madrid ya kupeleka ofay a pauni milioni 13 kwa
ajili ya De Gea inatokana na ukweli kuwa mlinda mlango huyo amebakisha mkataba
wa mwaka mmoja tu Old Trafford na kama Utd hawatamuuza sasa, itawawia kumruhusu
aondoke pasi na sumni msimu ujao.
Kama hiyo haitoshi, De Gea anasukumwa na ushawishi wa familia
yake akiwemo mpenzi wake ambaye maisha yake kwa kiasi kikubwa yapo nchini
Hispania ndani ya jiji la Madrid hivyo Madrid wanajua kwa vyovyote watamtia
mikononi De Gea.
De Gea aliyejiunga na Utd akitokea Atletico Madrid mwaka
2011 kwa uhamisho wa pauni milioni 17.8 tu, tayari ameshatoa mkono wa kwaheri kwa
wachezaji wenzake na kuweka wazi shauku yake ya kutaka kuelekea Hispania katika
majira haya ya joto na kuzipa mgongo pauni laki mbili (pauni 200,000)
alizotengewa kama mshahara endapo angesaini mkataba mpya na Utd na kumfanya awe
golikipa anayelipwa Zaidi ulimwenguni.
0 comments:
Post a Comment