Na Ramadhani Ngoda.
Ile
kauli ya ‘mwenye kisu kikali ndiye mwenye kula nyama’ inaonekana kutimia katika
vita ya kuwania huduma ya mlinzi wa kati wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya
Atletico Madrid, Joao Miranda ambaye amenyakuliwa na miamba ya Italia,
International Milan baada ya vilabu hivyo viwili kukubaliana ada ya uhamisho ya
pauni million 10.7 kwa ajili ya beki huyo.
Miranda
aliyekuwa akiwaniwa na miamba kadhaa barani Ulaya ikiwemo Manchester United ya
Uingereza, anatarajiwa kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa Inter baada ya
kumalizika kwa michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile akiiwakilisha
timu yake ya taifa ya Brazil.
Inter
Milan iliyo chini ya kocha Roberto Mancini ipo katika mchakato kabambe wa
marekebisho ya kikosi chake kabla ya kuanza kwa msimu wa 2015/16 wa ligi kuu
nchini Italia.
Taarifa
hii inaonekana kuwa pigo kwa Lius Van Gaal ambaye alikuwa akimwania Miranda ili
kuboresha safu yake ya ulinzi inayoonekana kusuasua tangu kuondoka kwa Nemanja
Vidic na Rio Ferdinand katika klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford jijini
Manchester.
Matumaini
pekee ya Van Gaal katika nafasi hiyo yanabaki kwa beki wa Real Madrid Raphael
Varane, Angelo Ogbonna (Juventus), Nicolas Otamendi anayekipiga katika klabu ya Valencia ya Hispania na mlinzi wa Borusia Dotmund Mats Hummels
0 comments:
Post a Comment