Baada ya taarifa kusambaa kwamba mshambuliaji wa
Yanga aliyetoroka, Mbrazil, Geinlson Santos Santana ‘Jaja’ anataka kurejea
klabuni hapo kutokana na kushindwa kulipa fedha za kuvunja mkataba,
Wanajangwani wamesema huo ni uamuzi wake.
Katibu mkuu wa Yanga, Dkt. Jonas Tiboroha amesema
kwamba Jaja alisaini mkataba, lakini alitoroka na wakaona njia nzuri ni
kumshitaki mahakamani kwasababu Tanzania sio shamba la bibi ambapo unakuja kuvuna pesa, halafu unaondoka.
Inaelezwa kwamba Jaja ameiambia Yanga kwamba fedha
wanazotaka alipe ni nyingi mno, hivyo anaona bora arudi kuitumikia klabu hiyo
msimu ujao wa ligi kuu soka Tanzania bara.
‘Huo ni uamuzi wake, Jaja alitolewa katika mazingira
yasiyoeleweka, alisaini mkatata, lakini akatoroka, hatuwezi kupoteza fedha
zetu nyingi kiasi kile, unajua wachezaji wa kigeni tunawalipa hela nyingi.
Unaajiriwa, unachukua fedha, halafu unatoroka kana kwamba Tanzania ni shamba la
bibi, unavuna hela na kuondoka
“Yanga tunataka alipe hela zetu au aje kuitumikia klabu,
bahati mbaya sana anaweza kuja na kukuta kanuni haziruhusu, atakuwa hana jinsi
zaidi ya kulipa fedha”. Ameeleza Tiboroha.
Kwasasa Yanga imeshajaza nafasi tano za wachezaji wa Kigeni ambao ni Kpah Sherman (Liberia), Andrey Coutinho (Brazil), Amisi Tambwe (Burundi), Haruna Niyonzima (Rwanda) na Mbuyu Twite (Rwanda), ingawa wanasubiri majibu ya mapendekezo yao waliyowasilisha TFF wakiomba idadi ya wachezaji wa kigeni iongezwa mpaka 10.
0 comments:
Post a Comment