MAMA wa
mchezaji nyota wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno Cristiano
Ronaldo ajulikanaye kama Doroles Aveiro alijikuta kwenye utata na vyombo vya
usalama katika uwanja wa ndege mjini Madrid mwezi uliopita, imefahamika.
Gazeti la del
mundo la nchini Hispania linaripoti kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 60
alikutwa na kitita cha dola 55,000 za kimarekani katika mkoba wake uwanja wa
ndege akijiandaa kuruka kwenda kwao nchini Ureno.
Pesa hizo ni
kinyume na sheria za wasafiri nchini humo kwani kiwango stahili kwa wasafiri
kubeba pesa wanapotoka nje ya nchi ni dola 10,000 tu za marekani.
Inaelezwa
kuwa mzazi huyo wa mchezaji bora wa dunia hivi sasa, hakujaza fomu zinazojazwa
kueleza sababu za kutoka na pesa zaidi ya dola 10,000 nje ya Hispania.
Watu wa
usalama wa kijamii katika uwanja huo wa ndege wakitimiza majukumu yao
walimtunzia mama huyo kiasi kilichozidi chote yaani dola 45,000 na kumruhusu
aendelee na safari.
Kwa mujibu
wa magazeti nchini Hispania, mtu anayekutwa na kosa hilo hutozwa faini
isiyopungua dola 600.
Mama huyo
ambaye amekua karibu sana na mwanae ‘Ronaldo’ wanaishi pamoja katika jumba la
kifahari mjini Madrid nchini Hispania, sambamba na mjukuu wake yaani mtoto wa
Cristiano.
0 comments:
Post a Comment