Uongozi wa Yanga, umemkabidhi mshambuliaji wake
mpya, Malimi Busungu jezi namba 16.
Straika huyo amejiunga na Yanga akitokea Mgambo
JKT ya Tanga.
Awali, Busungu alikuwa akiwaniwa na Simba, lakini
mwisho Yanga ilifanikiwa kumnasa.
Jezi hiyo ilikuwa ikivaliwa na Nizar Khalfani
aliyemaliza mkataba na Yanga, lakini uongozi umeamua kutomuongezea.
Nizar tayari ameshamwaga wino kuitumikia timu mpya
ya Mwadui fc.
Baada ya kukabidhiwa jezi hiyo, Busungu amesema
anaamini Yanga ni sehemu sahihi na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri.
0 comments:
Post a Comment