Khama Billiat |
TIMU ya taifa ya Malawi imechapwa 2-1 na Zimbabwe katika uwanja wake wa nyumbani kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2017).
Mabao ya Zimbabwe yametiwa kambani na Cuthbert Malajila dakika ya 23' na Khama Billiat dakika ya 83', wakati goli la kufutia machozi kwa Malawi limefungwa na David Banda dakika ya 24'.
Mechi nyingine zilizomalizika, Angola imeichakaza 4-0 Jamhuri ya Afrika ya kati.
Zambia ikiwa nyumbani imetoka suluhu (0-0) na Guinea-Bissau, wakati Nigeria imeshinda 2-0 dhidi ya Chad.
0 comments:
Post a Comment