Kuelekea mchezo utakaopigwa leo usiku kati ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Uganda ‘The Cranes’ makocha wa timu hizo jana walizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi waliyoyafanya kwenye vikosi vyao kabla ya pambano hilo kupigwa kwenye uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Kocha msaidizi wa Stars Salumu Mayanga amesema, kikosi chake kipo vizuri huku wachezaji wake wakiwa na ari ya kufanya vizuri kenye mchezo wa leo. Wakati huohuo kocha wa Uganda Micho mesema, wachezaji wake wapo kawenye hali nzuri na kuongeza kuwa Tanzania anaiju vizuri
Mchezo kati ya Stars dhidi ya Uganda unatarajia kuchezwa leo usiku majira ya saa 2:00 visiwani Zanzibar, huku mashabiki wa soka wa Tanzania wakiwa wamekata tama na timu yao mara baada ya kuambulia vichapo vinne mfululizo kwenye mechi zake za hivi karibuni.
Bofya hapa chini kusikiliza sauti zao;
0 comments:
Post a Comment