Liuzio akiwa kwenye vazi rasmi
MTANZANIA anayecheza
kandanda la kulipwa Zesco United ya Zambia, Juma Ndanda Liuzio
amekiri kusumbuliwa na ‘mademu’ wa Zambia kutokana na umaarufu wake wa
kutandaza soka.
Liuzio ni moja ya wachezaji
wa kutegemewa wa Zesco inayoshiriki ligi kuu ya Zambia na mara nyingi akiwa nje
ya uwanja hupenda kunyuka suti kali zinazomfanya awe na mvuto wa aina yake.
Liuzio (kushoto)
Akizungumza na MPENJA BLOG,
Liuzio amesema Wazambia wengi ni walevi na kuna changamoto nyingi za ujana,
lakini yeye anajali sana kazi iliyompeleka nchini humo.
“Changamoto za ujana zipo, kaka huku Wazambia ni walevi. Pia kuna kusumbuliwa
na wasichana, ila kikubwa ni wewe mwenyewe kujitambua. Amesema Liuzio na
kuongeza: “Mie huku nimekuja kufanya kazi , so hivyo vingine huwa navidharau tu, nafanya vile vilivyonifanya niwe hapa Zambia”.
0 comments:
Post a Comment