Monday, June 15, 2015

'Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein 'Tshabalala' ndiye beki pekee wa pembeni aliyeingia katika orodha ya wakali watatu kumsaka Mchezaji Bora wa msimu.'

MSIMU wa 2014/15 wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ulimalizika Mei 9 Yanga wakitwaa ubingwa huku Ruvu Shooting Stars ikiungana na Police Moro FC kuporomoka daraja.

Kuna wachezaji wengi waliofanya vizuri katika msimu huo. Katika mfululizo wa makala za kuangalia wachezaji wa VPL waliong'ara msimu mliopita, leo tunawaangalia mabeki tisa (9) wa pebeni waliofunika zaidi. Karibu...
 
1. KESSY RAMADHANI - MTIBWA/ SIMBA
Beki mkongwe Said Mkopi ameonekana wazi kushindwa kuziba pengo la Kessy katika kikosi cha Mtibwa Sugar tangu nyota huyo awahame mabingwa haoa mara mbili wa Tanzania Bara 1999 na 2000 na kujiunga na Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo Desemba mwaka jana.

Kessy ameudhihirishia umma kwamba ana uwezo mkubwa wa kucheza katika kikosi chochote akiwa beki wa pembeni kulia na kutekeleza kikamilifu jukumu la kulinda na kupandisha mashambulizi. 

Uwezo wake wa kukimbia kwa kasi, akili nyingi aliyonayo katika kuwakabili wapinzani na chenga zake za fedheha, unamuingiza katika orodha hii.

2. HASSAN MWASAPILI - MBEYA CITY
City imefungwa mabao 22 sawa na Tanzania Prisons. Timu hizo mbili zinakamata nafasi ya nne katika orodha ya timu zilizofungwa mabao machache zaidi msimu uliopita.

Ubora wa Mwasapili, beki wa pembeni kushoto, katika kulinda na kupandisha mashambulizi, umekisaidia kikosi cha Juma Mwambusi kumaliza nafasi ya nne katika msimamo wa VPL.

3. SHOMARI KAPOMBE - AZAM
Licha ya kufunga bao moja tu msimu uliopita, Kapombe amekuwa mpishi mzuri kwa magoli ya Mrundi Didier Kavumbagu na wakali wengine wa Azam FC. 

Kapombe amekuwa akitumiwa na Azam katika nafasi ya beki wa pembeni kushoto huku akilazimika kucheza nafasi ya beki wa kati kutokana na kuumia kwa Aggrey Morris na Pascal Wawa.

Kapombe pia ni miongoni mwa wachezaji wachache waliocheza mechi nyingi zaidi msimu huu, Wengine ni pamoja na Jacob Masawe wa Ndanda FC, Simon Msuva wa Yanga, Malimi Busungu wa Mgambo, kipa Said Mohamed na beki wa kati Salim Mbonde (wote wa Mtibwa Sugar).

Mafanikio ya Azam ya kumaliza nafasi ya pili VPL msimu uliopita, kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na ubora wa Kapombe. Kikosi cha 'Wanalambalamba' kilifungwa mabao 18 sawa na Yanga, zikiwa timu zilizofungwa mabao machache zaidi msimu uliopita.

4. SALUM KIMENYA - PRISONS
Kama ilivyodokezwa hapo awali, Prisons na City zimekamata nafasi ya nne katika orodha ya timu zilizofungwa mabao machache zaidi msimu uliopita.

Kimenya, beki wa pembeni kulia, amefanya kazi kubwa kuinusuru Prisons kuporomoka daraja. Beki alikuwa mpishi mzuri wa mabao ya 'Wajelajela'.

Kung'ara kwa winga Hamis Maingo katika kikosi cha Prisons ni wazi kumetokana ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa Kimenya.
 
5. HAMAD JUMA - COASTAL
Licha ya Coastal Union kufungwa mabao 25 sawa na JKT Ruvu, Juma alionyesha uwezo mkubwa katika kuwazuia mawinga wa timu pinzani walizokutana nazo. Juma ni miongoni mwa mabeki wachache wa pembeni kulia wanaotumia akili nyingi kukaba na kupandisha mashambulizi.

Changamoto kubwa inayomkabili Juma ni utovu wa nidhamu. Katika mechi yao waliyolala 1-0 dhidi ya Azam FC kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Machi 22, beki huyo alijifuta mikono yake kwenye soksi za refa msaidizi namba mbili (Line 2).

6. DAVID LUHENDE - MTIBWA
Aliachwa na Yanga kwa madai ya kushuka kiwango, lakini aliutumia vyema msimu uliopita kuwathibitishia Wanajangwani kwamba walikosea kutomwongeza mkataba.

Luhende alikuwa mwiba mkubwa kwa mawinga wa timu pinzani. Kasi yake katika kukimbia na kuchukua uamuzi, kupandisha mashambulizi na kutoa pasi za mwisho kunamuingiza Luhende kwenhye orodha hii.

7. YASIN MUSTAFA - STAND UNITED
Haongelewi sana na wadau wa soka nchini kutokana na kucheza katika timu isiyo na umaarufu mkubwa, lakini Mustafa ni miongoni mwa mabeki wa pembeni wenye ufundi mwingi uwanjani.

Stand ndiyo iliyofungwa mabao mengi zaidi msimu uliopita (34), lakini hili halimnyimi Mustafa fursa ya kuingia katika orodha hii kutokana na ubora alionao. Beki huyo ana nguvu, kasi na anatumia akili nyingi kukaba na kupandisha mashambulizi.

8. MOHAMED HUSSEIN - SIMBA
Watoto wa mjini wamepachika jina la Tshabalala. Nyota huyo amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Simba alichokiwezesha kumaliza nafasi ya tatu katika msimamo wa VPL msimu uliopita.

Ubora wa Hussein, Kessy na mabeki wa kati, Joseph Owino, Hassan Isihaka na Juuko Murshid ndiyo uliifanya ngome ya ulinzi ya Simba kuwa bora msimu uliopita. Timu hiyo ilifungwa mabao 19 ikiwa nafasi ya pili katika orodha ya timu zilizoruhusu nyavu zake kutikishwa mara chache zaidi.

9. JUMA ABDUL - YANGA
Abdul ni miongoni mwa wachezaji waliofanya kazi kubwa kuipa Yanga taji la 25 la Tanzania Bara. Alikuwa nguzo muhimu katika kuilinda timu yake isifungwe sanjari na kutekeleza kwa ufanisi mkubwa jukumu la kupandisha mashambulizi kupitia pembeni.

Abdul, beki wa pembeni kulia, pia alipika baadhi ya mabao ya Yanga. Kama ilivyo kwa Juma wa Coastal Union, Abdul alionyesha utovu wa nidhamu katika baadhi ya mechi. 

Katika mechi yao mwisho waliyolala 1-0 dhidi ya Ndanda FC mjini Mtwara, beki huyo alipigana na mchezaji wa zamani wa Simba, Paul Ngalema. Wote walitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu.

Abdul pia alimdhalilisha mmoja wa washambuliaji wa Etoile Sportive du Sahel (ESS) katika mechi ya Kombe la Shirikisho barani Afrika ambayo Yanga ililala 1-0 nchini Tunisia.

*IMEANDIKWA NA SANULA ATHANAS, MWANDISHI WA MICHEZO WA GAZETI LA NIPASHE.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video