Saturday, June 6, 2015

MIAMBA ya kandanda ya Hispania, FC Barcelona imefanikiwa kutwaa kombe la tano la Uefa Champions League baada ya kushinda 3-1 dhidi ya mabingwa wa Italia, Juventus katika mechi ya fainali iliyopigwa usiku huu uwanja wa Olympic, mjini Berlin, Ujerumani.
Barcelona walianza mchezo kwa kasi huku wakigongeana pasi za uhakika na katika dakika ya tatu, Ivan Rakitic aliandika bao la kwanza akimalizia pasi murua ya Andres Iniesta.
Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili Juventus walijipanga na kusawazisha goli hilo kupitia kwa Alvaro Morata aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa kutokana na shuti kali la Carlos Tevez.

Dakika ya 68' Lionel Messi alipiga shuti kali lililotemwa na kipa wa Juve, Buffon na mpira kumkuta Luis Suarez aliyefunga goli ta pili na la ushindi.

Dakika za nyongeza, Neymar akaifungia Barcelona goli la tatu kutokana na shambulizi la kushitukiza.
Barcelona chini ya Luis Enrique wamefanikiwa kutwaa makombe matatu msimu huu kwani awali walitwaa La Liga na kombe la Mfalme 'Copa del Rey'.
Hakika msimu wa 2014/2015 ulikuwa mgumu kwa walinzi wa timu za La Liga na Uefa Champions League kwasababu moto wa Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar Jr ni sawa na wa Petroli usiozimwa kwa maji.

TAKWIMU ZA MECHI YA LEO, BARCA KULIA, JUVENTUS KUSHOTO
statistics :
7
shots on target
8
8
shots off target
10
38
possession (%)
62
8
corners
6
1
offsides
0
24
fouls
12
2
yellow cards
1
14
goal kicks
9
1
treatments
1

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video