Klabu ya Liverpool imethibisha kumsajili mshambuliaji wa Burnley , Danny Ings licha ya klabu yake kushuka daraja msimu
uliopita.
Raia huyo wa Uingereza
mwenye umri chini ya miaka 22 ambaye mkataba wake umemalizika mwishoni wa mwezi
huu, atajiunga na Liverpool Julai 1 baada ya kukamilisha vipimo vyote vya afya.
Ings alikuwa na msimu
mzuri katika timu yake akipachika magoli 11 japo hakuweza kuisaidia timu yake
kukwepa mkasi wa kushuka daraja.
Mwanasoka
huyu anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na klabu ya Liverpool baada ya James
Milner kujiunga na Majogoo hao.
Ujio wake huenda ukawa unamaanisha ni mwisho wa
washambuliaji Mario Balotelli na Rickie Lambert ambao walishindwa kuonesha ubora baada ya
kusajiliwa msimu uliopita.
0 comments:
Post a Comment