Na Ramadhani Ngoda.
Kusuasua
kwa Liverpool msimu uliomalizika na kuondoka kwa Rafa Benitez katika klabu ya
Napoli kumempa Jurgen Klopp nafasi mbili za kazi baada ya kuiacha Dotmund
lakini Mjerumani huyo ameamua kujipa likizo isiyo na muda maalumu kabla
kufikiria kutafuta timu ya kufundisha.
“Nitapumzika mpaka ple ntakapoamua tena,” alisema Klopp.
Klopp(47)
amabaye ameiaga Dotmund aliyeitumikia kwa
miaka saba katika mchezo wa fainali
ya DFB-POKAL mwishoni mwa wiki na kuambulia kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa
Wolfsburg, amekuwa akihusishwa na kujiunga na Liverpool kurithi kiti cha kocha
wa sasa Brendan Rodgers aliyekuwa na msimu mbaya na Liverpool.
Nguli wa zamani wa Ujeruma Franz Backenbauer amemtaja Klopp kama mtu sahihi katika klabu ya Napoli baada ya Rafael Benitez kutimkia Santiago Bernabeu.
Kocha
huyo wa zamani wa Mainz awali aliwahi kutajwa kama mrithi wa Carlo Anceloti
aliyetimka Real Madrid, lakini Madrid wanatazamiwa kumtangaza Rafael Benitez
kama kocha mkuu wa klabu hiyo baadaye wiki hii.
Dortmund
watamkumbuka Zaidi Klopp kwa mafanikio yake Signal Iduna Park ikiwemo ubingwa
wa DFB-POKAL msimu wa 2011/12 na kutinga fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya
msimu wa 2012/13 walipoambulia nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment