Saturday, June 13, 2015


Timu ya watoto wa Kinondoni imefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuichapa Mara kwa mabao 2-1 ya mikwaju ya penalti.



Katika mechi hiyo safi kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, leo, timu hizo zilimaliza dakika za kawaida bila ya bao na kulazimika kuingia katika changamoto wa mikwaju ya penalti.


Mara walipata mkwaju mmoja kupitia nahodha wake na Kinondoni wakafunga miwili huku makipa wa pande zote mbili wakiokoa mikwaju miwili.


Kinondoni ilionekana kuwa na nafasi nzuri kuanzia kipindi cha kwanza pia cha pili, lakini hawakuzitumia vizuri.


Alliance na Ilala pia ya Dar es Salaam, ndiyo zimeingia fainali katika michuano hii ya kusaka timu ya watoto chini ya miaka 13 ambao wataingia kambini kwa ajili ya kuwaandaa vijana waliobainika kuwa na vipaji.


Programu hiyo imeandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Rais wake, Jamal Malinzi alikuwa uwanjani hapo kushuhudia mechi hizo mbili za kuvutia na ndiye alikuwa mgeni rasmi.


Source: Salehjembe

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video