KUTOKANA na kipigo cha magoli 3-0 walichopata Taifa Stars
dhidi ya Misri jana kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon 2017),
kocha mkongwe nchini, Abdallah Kibadeni ametaka benchi zima la ufundi kubomolewa.
“Mimi nilishasema kwenye vyombo va habari kwamba kuifunga Misri
labda kudra ya Mungu itokee, tukitaka kufanikiwa tujirekebishe kwanza, tuondoe
matatizo yetu, tufanye mambo ya ukweli.
Watu wanalia na benchi la ufundi, lakini wanang’ang’aniwa”. Amesema
kocha huyo wa zamani wa Simba na kuongeza: “Mpangilio mzima ni mbovu, uwezo wa
mwalimu ni mdogo, hajasaidia chochote, inaonekana hataki ushauri, hatuwezi
kufanya vizuri tukikaa na mtu asiyeshaurika. Kama mwalimu anashindwa aondoke,
watu wanaohusika na ufundi waondolewe, kipimo chetu sisi walimu ni mafanikio,
ukishindwa unaondonda”.
Kabadeni ambaye aliifikisha Simba fainali ya Kombe la CAF,
sahizi kombe la Shirikisho amesema imefika wakati wa kuwaamini makocha wazawa
ambao wanalijua vyema soka la Tanzania.
“Watafutwe wazawa hata wawili au watatu wafanye kazi ya
kututoa hapa tulipo na si kuendelea kuwaamini wageni wasiokuwa na msaada wowote”.
0 comments:
Post a Comment