Sakata la utata wa mkataba wa Ramadhan Singano 'Messi' na klabu yake ya Simba lipatiwe ufumbuzi kwa kuvihusisha vyombo husika.
Kauli hii imetolewa na kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibadeni wakati huu Messi anadai ana mkataba wa miaka miwili unaoisha Julai 2015 wakati Simba wanao wa miaka mitatu unaoisha Julai 2016
"Suala la Messi kuna kitu kimefichwa na lazima ukweli usemwe, mkataba anao Messi, TFF na Simba. Kuna vyombo vinajua sahihi ni yake au si ya kwake, kwanini vyombo visifanye kazi? lakini hapa inaonesha kuna watu wanatumia ujanja ujanja kupoteza ukweli. Wawe wakweli, ukweli unaweza kutusaidia kujua nini kilitokea"
"Kama kuna tatizo watu waje watizame umechakachuliwa au vipi. Messi amekulia pale ndani, lakini nataka haki itendeke". Amesema Kibadeni aliyewahi kumfundisha Messi kwa nusu msimu 2013/2014 kabla ya kutimuliwa na nafasi yake kuchukulia na Mcroatia Zdravko Logarusic.
0 comments:
Post a Comment